Header Ads

Fuvu la kichwa na mabaki ya mwili wa mwanafunzi vyakutwa shamba


GEITA: Fuvu la Kichwa cha na mabaki ya Mwili wa  Mwanafunzi Alex Pastory wa kidato cha kwanza shule ya sekondari ya Nyugwa  Wilayani Nyang’hwale Mkoani Geita vimekutwa katika shamba la Mwananchi  mmoja  huku sababu za kifo cha Mwanafunzi huyo zikiwa bado hazijajulikana. 

Akizungumza na  Waandishi wa  habari Kamanda wa Polisi Mkoani Geita Mponjoli Mwabulambo amesema marehemu wakati akiwa shuleni akiendelea na masomo kuna wakati aliomba ruhusa ya kwenda Nyumbani kwao ukerewa kwa madai ya kwenda kutibiwa na kutokana na hali yake ya afya kuwa nzuri ambapo alirudi February 28  mwaka huu na kuendelea na masomo.

Ameendelea kusema kwamba  tangu tarehe 1 mwezi machi  alitoweka shuleni shuleni na sehemu ambayo alikuwa amepanga kwani nyumbani kwao ni  Ukerewe na hivyo na ilipofika tarehe 8 mwezi huu kuna mwanamke alikuwa akilima shambani ndipo alipoona fuvu la Binadamu.  .Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hili ili kujua chanzo cha kifo

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.