Header Ads

Hizi ndizo sababu zinazo changia kupata maradhi ya ugonjwa wa figo
Na Jackline Victor kuwanda 
DODOMA: Matumizi ya vilevi kupita kiasi Imeelezwa kuwa ni miongoni mwa sababu zinazo changia kupata maradhi ya ugonjwa wa figo huku visababishi vya ugonjwa huo kwa kiasi kikubwa ni kutokana  vyakula vinavyoliwa.

Hayo yamesemwa na Naibu waziri wa afya maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Dkt Phaustine Ndugulile wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma katika siku ya maadhimisho ya  figo duniani, ambayo huadhimiwa kila mwaka ifikapo machi 14 huku  kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘’afya ya figo kwa kila mmoja ,kila mahali’’.


Mbali na hilo Dkt Ndugulile ameongeza kuwa matumizi ya dawa holela nayo yanachangia maradhi ya figo, kwani madaktari wanapo muandikia mgonjwa dawa hutambua tatizo la mgonjwa ni lipi ,wanajua dawa hizo zinawezaje kutibu tatizo hilo na kwa muda gani na madhara gani ambayo yanaweza kujitokeza kutokana na matumizi ya hiyo dawa.


Dkt Ndugulile amesema ugojwa wa kisukari na ugongwa wa presha ni miongoni mwa magonjwa ambayo yanachangia kwa kiasi kikubwa kuharibu figo.


Katika hatua nyingine amesema wananchi wengi wamekuwa hawana utaratibu wa kujua afya zao, hivyo, amewataka wananchi kuwa kuwa na utamaduni wa kuchunguza afya zao.


Kwa upande wake Daktari Bingwa wa magonjwa ya figo Dkt Onesmo kisanga amesema kuwa    Duniani kote asilimi kumi wanatatizo sugu la figo, kwani katika Afrika hali ni ngumu zaidi.


Nae Mkurugenzi wa kinga kutoka wizara ya afya maendeleo ya jamii,jinsia ,wazee na watoto Grace maghembe amesema matatizo haya yamekuwa yakitokea sana mijini ni kutokana na mfumo wa maisha ambao watu wamekuwa wakiishi.


Hatahivyo, Ndugulile amesema mtu yeyote anaye umwa  anaenda hospitali   anatakiwa kuzingatia misingi ya zile dawa ambazo anazo, hatakiwi kuongeza dozi kuamini kwamba atapona haraka na wala asirefushe matumizi ya dozi na hususani matumizi ya dawa za kupunguza maumivu kwani zimekuwa zikitumika  vibaya kwa kiasi kikubwa,
Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.