Header Ads

Idadi ya waliofariki yafikia watu 50 New Zealand


Watu wa New Zealand walimiminika katika maeneo ya kumbukumbu na kuweka maua na kuomboleza wahanga wa mauaji katika misikiti miwili.

Wakati hayo yakifanyika ushahidi ulijitokeza machungu ya mateso katika  mashambulio ya bunduki ambayo yalichukua maisha ya watu 50.

Kamishna wa polisi Mike Bush amesema maafisa waliweza kuwapatia familia orodha ya wahanga, kitu kilichocheleweshwa kutokana na haja ya kazi ya tahadhari ya polisi  pamoja na kiwango cha  mkasa  huo, Kwa muda wa karibu siku  tatu timu za uchunguzi wa alama katika matukio ya uhalifu, wengi wakiwa wamekuja kutoka sehemu mbali mbali za New Zealand, wamekuwa wakifanyakazi  katika maeneo kadhaa  ya uhalifu, katika misikiti ya Al Noor na Linwood pamoja na nyumba katika  eneo  la  Dunedin, mji wa  kusini  mashariki  ambako  mtu anayeshukiwa kuwa ndie aliyefanya  mashambulizi ya bunduki.

Tayari matrekta ya kuchimba yameanza kazi katika eneo la makaburi  mjini humo kuondoa mchanga unaohitajika kwa ajili ya kuwazika wahanga waliofariki.

Mara  utambulizi utakapokamilika  majina yatatangazwa, Bush alisema. Lakini  tayari taarifa za  wahanga  kutoka  katika mataifa ya Kiislamu zimeanza  kuonekana.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.