Header Ads

Jamii yashauriwa kuacha kutumia dawa kiholela


DODOMA:IMEELEZWA kuwa takribani watu laki saba hufariki kila mwaka duniani kote  kutokana na tatizo la usugu wa vimelea vya magonjwa  vinavyotokana na matumizi holela ya dawa.

Hayo yameelezwa Jijini Dodoma na Mtendaji Mkuu wa shirika lisilo la kiserikali RBA INITIATIVE,ERICK VENANT    ambaye pia ni mfamasia wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na madhara yatokanayo na usugu wa vimelea vya magonjwa.

Akieleza zaidi VENANT amesema kuwa ,vifo hivyo hutokana na  matumizi holela ya dawa ambapo watu hutumia bila kufuata ushauri wa wataalamu wa afya na kusababisha Dawa kushindwa kutibu maambukizi hata ya kawaida.


Aidha Mtendaji huyo amefafanua kuwa hali hiyo hupelekea dawa kushindwa kufanya kazi na kushindwa  kutoa matokea yanayotarajiwa katika mwili wa binadamu ambapo vimelea vya magonjwa ndio vinakuwa sugu dhidi ya dawa.

  
Licha ya hayo ameongeza kuwa tatizo hilo linaleta madhara katika sekta za binadamu,mifugo na hata mimea,na kusababisha dawa kushindwa kutibu ipasavyo.

Pia ameishuri Jamii kuacha mazoea ya kutumia dawa za binadamu au za mifugo kiholela bila kutafuta na kufuata ushauri wa kitaalamu ikiwa ni pamoja na kuzingatia kanuni za usafi ili kuzuia kusambaa kwa vimelea vya magonjwa kote katika sekta za binadamu na mifugo.

 Hata hivyo amesema, wao kama shirika linalojikita katika kutoa elimu ya kutokomeza usugu wa vimelea vya magonjwa wamekuwa wakifanya juhudi mbalimbali  katika sekta za afya ya binadamu,mifugo na mazingira ili kutatua tatizo hilo.


Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.