Header Ads

Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini yapongeza mradi wa umeme Makambako-Songea.


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, chini ya Mwenyekiti, Mariamu Ditopile Mzuzuri, imeipongeza Serikali kwa kutekeleza mradi wa umeme wa Makambako- Songea (kV 220) ambao umewezesha Mikoa ya Ruvuma na Njombe kupata umeme wa uhakika kutoka Gridi ya Taifa.

Kamati hiyo, imetoa pongezi hizo wilayani Songea, Mkoa wa Ruvuma, baada  ya kukagua utekelezaji wa mradi huo ambao umehusisha ujenzi wa njia ya umeme ya msongo kV 220 kutoka Makambako hadi Songea, ujenzi wa Vituo vya kupoza umeme vya Makambako, Madaba na Songea na usambazaji umeme katika Vijiji 122.

Kabla ya  kukagua kituo cha kupoza umeme cha Songea, Kamati hiyo ilikagua vituo vya Makambako na Madaba pamoja na njia ya usafirishaji umeme kutoka Makambako hadi Songea ambapo watendaji mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), walihudhuria.

Pamoja na pongezi hizo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, aliiagiza Wizara pamoja TANESCO kuhakikisha kuwa, wanapeleka umeme katika Vijiji vyote vilivyopangwa kupelekewa umeme kupitia mradi huo na kutoruka kijiji chochote ambacho kimepitiwa na mradi.

Aidha, aliiagiza Wizara ya Nishati na TANESCO kuhakikisha kuwa, inahamasiha wananchi kutumia umeme huo kwa matumizi mbalimbali ikiwemo ya viwandani kwani mikoa hiyo sasa ina umeme wa kutosha na wa uhakika na Serikali inahitaji wateja wengi zaidi ili kuongeza mapato.

Awali, katika kituo kupoza umeme cha Makambako, Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani aliieleza Kamati hiyo kuwa, mradi huo umekamilika mwaka 2018 na kazi inayoendelea sasa ni usambazaji wa umeme katika Vijiji vya awali 122 ambapo Vijiji 105 tayari vimesha unganishwa na nishati hiyo

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.