Header Ads

Kisanduku cheusi cha ndege ya Ethiopia kutumwa nje ya nchi


Kisanduku cheusi kutoka kwenye ndege ya Boeing ya Shirika la ndege la Ethiopia iliyoanguka na kuwauwa watu 157 abiria wote pamoja na wafanyakazi kitatumwa nje ya nchi kwa ajili ya uchunguzi lakini hakuna nchi ambayo imekwisha teuliwa.

Msemaji wa Shirika hilo la ndege Asrat Begashaw ameliambia shirika la habari la AP kuwa wana mambo kadhaa ya kufanya kwa ajili ya data na sauti zilizorekodiwa wakati wa dakika za mwisho za ndege hiyo kabla ya kuanguka lakini amesema kuwa Ethiopia haina uwezo wa kuufanya uchunguzi huo.

Ndege hiyo ya Boeing 737 Max 8 ilianguka muda mfupi baada ya kuondoka uwanja wa ndege wa Ethiopia Jumapili asubuhi kuelekea Nairobi na kuwauwa watu wote 157 waliokuwemo.

 Wakati huo huo, nchi nyingi kote duniani zimesitisha matumizi ya ndege za Boeing 737 Max 8, ikiwa ni pamoja na Umoja wa Ulaya. Marekani ni mojawapo ya nchi chache zinazoendelea kuitumia ndege hiyo.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.