Header Ads

kitu cha mwisho ambacho alikiposti Ephraim Kibonde

Hiki Ndicho  kitu cha mwisho kupost Ephraim Kibonde
Ikiwa ni masaa machache tangu mtangazaji pendwa wa Clouds FM, Ephraim Samson Kibonde kufariki dunia, imeonekana kama moyoni mwake alimkumbuka sana mke wake ambaye kwa sasa ni marehemu.


Kibonde alituthibitishia hilo kupitia ukurasa wake wa instagram, baada ya kumpost picha ya marehemu mke wake, siku tatu nyuma kabla ya kufariki dunia, bila kuandika ujumbe wowote.

A post shared by Ephraim Kibs (@ephraimkibonde) on Mar 3, 2019 at 3:54pm PST

Kibonde alifiwa na mkewe Julai 2018, kitu ambacho mwenyewe alikiri kuwa ndio tukio kubwa lililoumiza moyo kwenye muda wote wa maishani mwake, kutokana na jinsi alivyokuwa karibu na mke wake, na kuwa kama rafiki yake kutokana na upendo ambao alikuwa nao.

Ephraim Kibonde ameacha watoto watatu, Junior,Hilda na Ilaria, ambao kwa sasa watakuwa wamebaki yatima kwa kumpoteza na baba yao pia. 

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.