Header Ads

Mapigano Burkina Faso yawaathiri wanafunzi 150,000 kwenda shule


Mashambulio ya wanamgambo na mapigano ya kijamii kaskazini mwa Faso yamewazuia watoto 150,000 kuenda shule.

"Shule nyingi zimechomwa moto, walimu wameshambuliwa na baadhi yao kuuliwa," anasema mmoja wa wakuu wa shule hizo, Samuel Sawadogo.

"Mwalimu anapouawa, hakuna hatua yoyote inayochukuliwa, kwa hivyo inabidi tujiokoe sisi wenyewe."

Zaidi ya watoto 150,000 wameathiriwa na hatua ya kufungwa kwa shule hizo.

Bwana Sawadogo anasema vikosi vya usalama vimeshindwa kuwahakikishia usalama wakaazi wa maeneo hayo, lakini ana matumaini kuwa shule zitafunguliwa hivi karibuni.

Shule kadhaa katika maeneo yaliyoathiriwa na kutapata taswira ya kamili ya kwanini shule zimefungwa au kwanini madarasa hayana wanafunzi.

Baadhi ya shule hasa katika mkoa wa Sahel zinalengwa na wanamgambo wa kiislam ambao wanapinga ''elimu ya magharibi.''

Zingine zilizo katika mji wa unaofahamika kama Foubé, zimefungwa na waalimu ambao wanahofia huenda wakashambuliwa

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.