Header Ads

Marekani yatarajia mazungumzo na Rais wa Korea Kaskazini


Marekani inaelezea matumaini ya kuendelezwa mazungumzo ya kusitishwa silaha za nyuklia pamoja na Korea ya kaskazini.

 Matamshi hayo ameyatoa waziri wa mambo ya nchi za nje Mike Pompeo kufuatia ripoti kwamba Korea ya Kaskazini inazingatia uwezekano wa kusitisha mazungumzo hayo.

 Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Mike Pompeo amesema pia anataraji kiongozi wa Korea ya kaskazini Kim Jong Un atatekeleza ahadi zake za kutoanza upya majaribio ya makombora na silaha zake za nyuklia.

 "Ni matumaini yetu kuona mazungumzo yanaendelezwa katika suala hilo" amesema waziri huyo wa mambo ya nchi za nje wa Marekani.

 Maafisa wa Marekani walisema wako tayari kwa duru nyingine ya mazungumzo baada ya duru ya pili kati ya rais Donald Trump na kiongozi wa Korea ya Kaskazini Kim Jong Un kuvunjika bila ya makubaliano mwezi uliopita mjini Hanoi na bila ya kutolewa sababu halisi.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.