Header Ads

Mavunde aitaka kampuni ya G Tech Kusaidia suala la ulinzi na usalama Jijini Dodoma


DODOMA:Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana ANTHONY MAVUNDE ameitaka kampuni ya G-Tech inayojishughulisha na masuala ya teknolojia ya habari na mawasiliano kuhakikisha wanasaidia katika suala la ulinzi na usalama katika jiji la Dodoma kutokana na kasi ya ukuaji wake.

Mavunde ambaye ni mbunge wa jiji la Dodoma ametoa rai hiyo jijini Dodoma wakati akizindua ofisi ya Kampuni hiyo ambapo amesema  jiji la Dodoma linakua kwa kasi hivyo matumizi ya teknolojia yanapaswa kuongezeka hasa katika maeneo ya ulinzi na usalama.


Ameipongeza kampuni hiyo kwa kutoa ajira kwa vijana na kusema serikali inaunga mkono jitihada zozote  zinazofanywa katika kuongeza ajira kwa vijana na kuwakwamua kiuchumi.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo SALIM MUSSA OMARY amesema wamejikita kutoa huduma za habari na mawasiliano na walianza na uwekaji wa kamera za CCTV barabara za Zanzibar.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.