Header Ads

Mbinu itakayokufanya ukue kibiashara ili upate faida ni hii


U hali gani mpenzi msomaji wa  mtandao huu bila shaka u mzima na unaendela vyema na majukumu yako ya kila siku, naomba nichukue wasaa huu  nikukaribishe siku ya leo ili tuweze kujifunza kwa pamoja mbinu moja ya muhimu ambayo itakufanya ujiongee thamani na wateja kwa ujumla katika biashara unayofanya.

Nimekuletea mbinu hii  moja muhimu kwa sababu nimegundua  ya kwamba ni mbinu ambayo imekuwa ikiwasaidia wafanyabiashara wengi wakubwa kwa wadogo, ambao wamekuwa wakiiitumia mbinu hiyo.

Naomba pia niwe muwazi kwako kama endapo  mbinu hiyo haitukusaidia endapo utaamua katika biashara yako naomba tuwasiliane nipo  tayari kurudisha kiwango cha Mega bites(Mb) zako ambazo utatumia kusoma makala hii.

Pasipo kupoteza muda mbinu hiyo ni kutoa ofa kwa wateja wako au ‘promotion’ kama wengi wanavyopenda kuita.

Kanuni hii kwa mfanyabishara mdogo anaweza akasema labda kanuni hii hamhusu ila ukweli ni kwamba kanuni hii ni nzuri sana kwa mfanyabishara mdogo na mfanyabishara mkubwa pia, hii ni kwa sababu mbinu hii ina mashiko sana katika kuikuza biashara yako.

Hata ukifanya uchunguzi wako usio rasmi utagundua makampuni yaliyo mengi yana ushindani mkubwa katika jambo hili  la utoaji wa ofa, yaani wengi wao wamekuwa wakiishinda kuleta ofa mbalimbali mpya  zitakazowavutia wateja wa zamani na wateja wapya.

Na katika ofa hizo huendana na maneno mazuri yenye kuleta hamasa za kumvutia mteja, wapo ambao utawasikia wanasema ya kwamba jaza ujazwe, wapo wengine ambao husema onja msimumuko, wapo wengine husema jipimie, wapo wengine husema usipoelewa utarudishiwa ada yako na maneno mengine kama hayo.

Yupo mfanyabishara mwingine nimewahi kukumbana na bango dukani kwake lenye maneno yanasomeka hivi “ ofa ofa piga picha mbili kwa bei ya moja” mwisho wa kunukuu. Kwa maneno kama haya unadhani mteja hawezi kwenda kweli? Naomba majibu ya swali hilo uyaweke ‘password.’

Hivyo haijalishi ni biashara ndogo au kubwa ni vyema kuna wakati  uweze kutoa ofa kwa wateja wako na katika kutoa ofa hii ni lazima uzingatie ya kwamba ni lazima iwe ofa ambayo haitakuletea maumivu makubwa katika biashara yako, bali iwe ni ofa ambayo itakuongezea faida kwani siku zote ikumbukwe  utoaji wa ofa katika biashara huleta faida.

Mwisho nisikuchoshe kwa maneno mengi, kwani maneno mengi hayavunji mfupa bali nikwambie ya kwamba biashara ili iweze kwenda vizuri inahitaji pia ni ofa na ofa huleta faida na wateja kemkem. Hivyo walau kwa mwaka ukiweka ofa moja katika biashara yako basi itapendeza zaidi.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.