Header Ads

Mc Pilipili ataja mwezi wa kufunga harusi, adai kutakuwa na kiingilio

Mc Pilipili ataja mwezi wa kufunga harusi, adai kutakuwa na kiingilio
Mipango ya harusi ya mshereheshaji Emmanuel Mathias maarufu ‘MC Pilipili’, imepamba moto, huku ikitarajiwa baadhi ya wageni kulipia Sh.10,000 ili kuhudhuria.

Akizungumza leo, MC Pilipili ambaye pia ni mchekeshaji, amesema harusi hiyo inatarajiwa kufanyika baada ya Sikukuu ya Pasaka na itakuwa na kiingilio kitakachoanzia Sh10,000 kwa watu wa kawaida.

Amesema amefikia hatua ya kuweka kiingilio kwa kuwa hadi sasa watu wanaotaka kuhudhuria harusi hiyo ni wengi na ili kutowakosesha wengine haki ya kuiona, ameona ni bora kuweka kiingilio.

”Mpaka ninavyoongea na wewe hapa watu ni wengi sana wanaotamani siku hiyo ifike waweze kushuhudia na mimi nimeona nisiwanyime hiyo nafasi bila kujali uwezo wao kifedha, naamini kiingilio hicho kitawafaa kushiriki nasi na kusherekea siku hiyo muhimu katika maisha yetu na mke wangu mtarajiwa,” amesema.

Mshereheshaji huyo Januari mwaka huu aliibua gumzo mtandaoni baada ya kuonekana akilia wakati wa hafla ya kumvisha pete mchumba wake, Philomena Thadey

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.