Header Ads

Mkuu wa mkoa wa Tabora azindua jukwaa la sitetereki


Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amezindua jukwaa la 'Sitetereki' likiwa na lengo la kutoa elimu ya afya na kundi rika kwa vijana na amehimiza mabadiliko kwa jamii kwa kuwalinda vijana.

"Vijana wetu inafikia mahali wanapata mshawasho lakini anajua ni kwa nini anakuwa hivyo kwenye kipindi hiki anakiita barehe pale ni mahali pakumlea na kumtunza, haiwezekani watoto wanakwenda wanavurugwa vurugwa na kutupwa kwenye mtaro majamaa wameshakadandia," RC Mwanri.

“Hapa tunazindua jukwaa la Siteteleki  vijana nia asilimia stini hapa ninchi na niyakwanza katika bala la afrika kwakua vijana wengi, zaidi ya asilimia hamsini vijana wapo katika mahusiano Kama rafikiyako hakufai mpige sendiofu achana nae hana faida’’ amesema Mwanri.

Aidha Mwanri amesema kuwa kinachowaletea vijana matatizo ni kampani waliyonayo huku akisema wanapenda kuambatana na marafiki na kuwakumbatia hata kama wanawapeleka kwenye makorongo.

Mwanri ameyasema hayo katika jukwaa la mawasiliano ya  afya  kwa vijana la Sitetereki Mganga mkuu mkoa wa Tabora Honoratha Rutatinisibwa, lililofanyika mkoani Tabora  likiwa na lengo la kumsaidia kijana kufikia malengo yake kwa na kumuelimisha kwa masuala ya afya jambo ambalo litaweza kuwasaidia vijana kuondokana na dhana potofu.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.