Header Ads

Mwanafunzi afa maji akiwa anaogelea mto kiwira


Mwanafunzi wa Chuo cha Ualimu Tukuyu Mwaka wa Tatu aitwaye Samwel James Chacha (25) amekufa maji akiwa anaogelea kwenye Mto Kiwira uliopo Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya.

Tukio hilo lilitokea Machi 7, mwaka huu na  jitihada za kuutafuta mwili wa mwanafunzi huyo
zilifanyika. Mwili wa marehemu ulipatikana Machi 11 mwaka huu majira ya saa 10 jioni katika Kijiji cha Mboyo, Kata ya Lupepo, Tarafa ya Ukukwe, Wilaya ya Rungwe na Mkoa wa Mbeya kwenye mto kiwira.

Taarifa ya Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya imeeleza chanzo cha tukio ni uzembe wa marehemu kutaka kuogelea kwenye mto huo bila kuchukua tahadhari. Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Rungwe –  Makandana kusubiri uchunguzi wa kitabibu

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.