Header Ads

Mwinyi zahera akanusha taarifa hizi


Kocha mkuu wa Yanga SC, Mwinyi Zahera amekanusha taarifa zilizodai fedha za michango zinazotolewa na wanachama kwaajili ya kusaidia timu zinaliwa na viongozi.

Zahera amesema kuwa hayo maneno sio ya kweli kwasababu pesa zote zinazoingia wanashirikishwa matumizi yake.

"Kuna watu wanashambaza hizi taarifa ili wanachama wetu wasichangie, timu yao ipate matatizo lakini kiukweli hakuna hata elfu moja ambayo imeibiwa zote zinatumiaka vizuri na wala viongozi hawazichukui'', amesema.

Katika hatua nyingine nahodha Ibrahim Ajibu amesema kuwa ni shuhuda namba moja wa matumizi ya pesa hivyo kwani kila pesa inayotoka ni lazima waidhinishe yeye na kocha.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.