Header Ads

Namna ya kupata mafanikio kwa muda muafaka lakini zingatia haya

Kuna baadhi ya watu huelekeza mawazo yao hasi katika kulaumu watu wengine kuliko kuwaza ni kwa jinsi gani wataweza kuyasaka mafanikio kiurahisi kabisa. Tunatumia muda mwingi katika kufanya mambo amabayo hayana manufaa katika Maisha yetu. Kwa kuwa tunapoteza muda huo mwingi katika mambo yasikuwa na tija inafika mahali tunakuwa watu wa maisha ya kawaida kila siku.

Hivyo zifutazo ndizo mbinu za kuapata mafanikio unayoyataraji ndani ya muda mfupi:

1. Siyo kila unachokisia ni lazima ukifanyie kazi.
Kimsingi maneno ya watu yapo ambayo yanajenga kwa namna moja ama nyingine, Ila yapo  maneno mengine ambayo hayaajengi, na haya  ndiyo yapo mengi zaidi, kwa mfano leo hii ukitaka kufanya biashara utakwenda kumshirikisha mtu ambaye yupo karibu yako, unakwenda kuomba ushauri, mtu huyo atakwambia biashara hiyo hafai, mwishowe unajikuta unabadilisha mawazo na kufanya jambo jingine na kwa kuwe wewe haujimijini unajikuta  hakuna hata jambo hata moja ambalo unalifanya kwa uhakika.

Hivyo daima ukumnbuke mafanikio ni maamuzi ya mtu mwenyewe, hivyo unatakiwa wakati mwingine kufanya maamuzi yako binafsi kabla ya kuomba ushauri kwa watu wengine.


2. Tambua kusudio lako.
Moja ya changamoto ya watu wengi ambao walifeli kimaisha ni kwamba watu hao walifanya vitu bila kujua ni nini kusudio lako?, kitendo hiki kikawapelea watu hao kuweza kuwa na malengo ambayo hayana tija. Unakuta mtu anafanya biashara ukimuuliza kusudio la kufanya biashara hiyo utakushanga ya kwamba hata mfanyabiashara huyo huenda ukawa hajui pia.

hivyo kila wakati unahitaji kuwa na picha kamili ya jambo ambalo unalifanya kwa miaka ya mbeleni. Picha hii ndiyo ambayo itakuonesha utaweza kufanikiwa kwa kiasi gani? Au utafeli kwa kiasi gani. Kama ni biashara ni lazima uwe na mlolongo mzima wa biashara yako.

Amini nguvu iliyipo ndani yako kwamba unaweza.
Watu wengi hawaamini nguvu ambazo zipo ndani yao. Wengi huamini ya kwamba Mafanikio huja kwa watu wachache waliobahatika, la  hasha ikumbukwe kwamba  Mafanikio yapo kwa kila mtu ambaye anamini ya kwamba yeye ni mshindi katika maisha yake, bila kuangalia ni changamoto ngapi ambazo amezipitia. Pia ikubukwe kujua nafasi uliyonayo katika jamii hii, pia ni lazima ujiulize ya kwamba unaitumia vipi nafasi uliyonayo. Mwisho kujua  wewe wako ndio siri ya Mafanikio kwani moja ya watu wengi walifeli katika Maisha ni kwamba waling'ang'ana kufanya vitu visivyokuwa vya kwao. Nikuache na swali la kujiuliza je jambo ambalo unalifanya ni lako?

Maisha ya mwanadamu hususani katika kipengele cha mafanikio ni lazima yafanane  na miiba ya michongoma kwa maana ya kwamba kila wakati uwe tayari katika kupambana na changamoto ambazo zinajitokeza kama ilivyo kwa miiba ya michongoma, maana miiba hii kila wakati upo  tayari kwa ajiri ya upambanaji tu.

Mwisho Afisa nimalizie kwa kusema akili ikiamua kufanya jambo inawezekana hivyo inahitajika nguvu ya mwili katika kuisaidia akili katika utekelezaji.

Na. Benson Chonya.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.