Header Ads

Ni wakati wa viongozi wa afrika kuiangalia afrika ijayo-Samia


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema huu ni wakati Viongozi wa Afrika kuiangalia Afrika ijayo hivyo hakuna budi viongozi wa sasa kuandaa mazingira ya Afrika bora na salama.

Makamu wa Rais ameyasema hayo kabla ya kumalizia sehemu ya mwisho ya Mkutano wa Africa Now Summit 2019 unaofanyika kwenye hoteli ya Munyonyo Commonwealth Resort, Kampala nchini Uganda.

Makamu wa Rais amesema mkutano huo umeangalia suala zima la ongezeko la watu na uelewa wa vijana katika maendeleo ya nchi zao haswa wakati huu wa uchumi wa viwanda ambapo pia kuangalia mitaala ya elimu inayotolewa sasa kama inakidhi mahitaji ya kisayansi na kiteknolojia.

"Lazima sasa tuangalie hii idadi ya watu isije ikawa chanzo cha kuleta vurugu katika nchi zetu bali iwe chanjo cha nguvu kazi kujenga nchi zetu”alisema Makamu wa Rais.

 Makamu wa Rais amesisitiza kuwa Afrika ya sasa inahitaji Viongozi ambao hawajitazami wao bali wanatazama wananchi wao katika makundi yao kama Vijana, Wanawake na Walemavu.

Makamu wa Rais pia alikutana na kuzungumza na Naibu Rais wa Kenya Mhe. William Ruto ambapo baada ya kikao hicho Makamu wa Rais amesema Tanzania na Kenya ni majirani pamoja na kuwa kwenye jumuiya ya Afrika Mashariki lakini wao kama nchi jirani lazima wahakikishe uhusiano wao unasimama imara na kukuza ushirikiano.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.