Header Ads

Serikali ya awamu ya tano yadhamiri kuwezesha wananchi


Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Uongozi wa Rais, Dkt.  John Pombe Magufuli imedhamiria kwa dhati kuwawezesha wananchi kujenga uwezo wa kujitegemea kiuchumi tangu ilipoingia madarakani mwaka 2015.

Dhamira hii safi imekuwa ikitekelezwa kwa vitendo   na  Serikali, Tumeshuhudia  Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA)  unavyoendeleza azma hii  kwa kujenga uwezo kwa wananchi ili watumie ardhi kujikwamua kiuchumi kama azma ya ya Serikali yetu ilivyo.

Mpango huu wa MKURABITA umejikita katika kuwawezesha wananchi wanyonge ili waongeze tija na kuchangia katika ujenzi wa uchumi na hasa kujenga Taifa linalojitegemea na lenye wananchi wanaoshiriki kumiliki uchumi unaotokana na rasilimali zilizopo katika maeneo yao.

Jukumu kubwa linabaki kwa wananchi  kuunga mkono Serikali ili juhudi hizi zakuwakwamua kiuchumi  zizae matunda kwa wakati ili Tanzania ifikie azma ya kuwa nchi ya asali na maziwa kama alivyodhamiria Mhe. Rais wetu Dkt. John Pombe Magufuli.

Wananchi katika maeneo mbalimbali hapa nchini wamenufaika na urasimishaji wa ardhi yakiwemo mashamba, kwa mfano katika Wilaya ya Chamwino tumeona uwezeshaji ukifanyika kwa wakulima wa vijiji vya Mahama na Membe, lengo likiwa ni kuwawezesha wananchi hawa kutumia hatimilki za kimila za kumiliki ardhi kujikwamua kiuchumi.

Rai kwa wananchi ni kuendelea kuiunga mkono Serikali ya Awamu ya Tano katika jitihada zake za kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa nchi ya kupigiwa mfano kupitia mipango mbalimbali inayotekezwa ukiwemo huu wa urasimishaji rasilimali na biashara za wanyonge.

Mpango huu una faida lukuki kwa wananchi, nampongeza Mhe.  Rais kwa kuendelea kuweka mkazo katika masuala yote yanayolenga kuwawezesha wananchi hasa wanyonge vijijini ili waweze kufurahia na kujikwamua kiuchumi kupitia rasilimali zilizopo ikiwemo ardhi .

Urasimishaji ardhi hasa vijijini ni kichocheo cha maendeleo na umekuwa na faida nyingi, baadhi yake ni kuwasaidia wananchi kuwa na umuliki ardhi unaotambulika kisheria, uhakika wa usalama wa milki ya rasilimali ardhi zinazomilikiwa huko vijijini, kupunguza migogoro ya ardhi, kuongeza thamani ya ardhi husika, kutumia hatimilki za kimila kujipatia mitaji kupitia katika taasisi za fedha.

Kwa upande wake mratibu wa MKURABITA, Dkt. Seraphia Mgembe amesema kuwa dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano kupitia mpango huo ni kuhakikisha kuwa inawawezesha wananchi kushiriki katika kujenga uchumi na kuwa na uwezo wa kumiliki rasilimali zilizopo katika maeneo yao.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.