Header Ads

Simba SC yapania point 3 kutoka JS Saoura

Wakati kikosi cha timu ya Simba SC  kikiwa katika maandalizi ya mwisho kuelekea mechi ya marudiano na JS Saoura huko Algeria Machi 9 wiki hii, imeelezwa hali ya hewa huko Algiers ni shwari na imeongeza morali kwa wachezaji wa kikosi hiko kuibuka na ushindi.

Simba wamefika  Algiers na kuweka kambi ya muda kuendelea na mazoezi dhidi ya JS Saoura wakiwa na kumbukumbu ya kushinda mabao 3-0 Uwanja wa Taifa, Dar magori yaliyofungwa na Emmanuel Okwi 45+3', na Meddie Kagere 52', 67'.

Hali hiyo ya hewa inaweza ikawa msaada kwa Simba katika mechi ya Jumamosi kwani kiafya haiwezi ikawaathiri wachezaji wake.

Simba itaingia dimbani kucheza na Saoura ambapo mechi hiyo itaanza majira ya saa 4 kamili za usiku kwa saa za Afrika Mashariki huku wakiwa na kumbukumbu ya kuishinda Al Ahaly ya Misri kwa bao 1 kwa 0.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.