Header Ads

Uingereza huenda ikashiriki uchaguzi wa bunge la Ulaya


Uingereza italazimika kushirika kwenye uchaguzi wa bunge la umoja wa Ulaya, iwapo mchakato wa kujiondoa kwake kutoka umoja huo utapindukia Julai mosi mwaka huu.

Hayo yamesemwa na mjumbe wa Austria kwenye mazungumzo ya Brexit Gregor Schusterschitz katika mahojiano yaliyochapishwa leo na gazeti moja la nchini Austria.

Mwanadiplomasia huyo amesema Umoja wa Ulaya, haujawahi kuwa kikwazo kwenye majadiliano ya Brexit, na hakuna sababu ya Uingereza kunyimwa muda zaidi kufanikisha Brexit.

Waziri mkuu Theresa May anatarajiwa kwenda Bressels baadae wiki ijayo, kutoa pendekezo la kuchelewesha mpango wa nchi yake kuondoka muungano wa Ulaya.

 Hiyo ni baada ya Bunge la Uingereza kupiga kura siku ya Alhamisi, kurefusha muda wa majadiliano baada ya Machi 29 tarehe ambayo Uingereza ilipaswa kuondoka kutoka Umoja wa Ulaya

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.