Header Ads

UVCCM wapatiwa elimu ya masharti ya kuomba mkopoVijana  wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya Rorya mkoani Mara wamepatiwa elimu juu ya masharti ya kuomba mkopo kutoka halmashauri wa asilimia 10 inayotokana na makusanyo ya mapato ya ndani.

Afisa maendeleo ya Jmaii wilaya Rorya,Majula Mgeta alisema jana katika kikao cha Baraza la UVCCM wilaya Rorya kilichokalia ukumbi wa CCM Utegi kuwa na kuwashirikisha Mbunge wa jimbo hilo,Lameck Airo pamoja na mwenyekiti wa CCM Wilaya Rorya,Charles Ochere kuwa halmashauri yake imekasimia   shilingi milioni 98 kwaajili ya mikopo ya wanawake,Vijana na walemavu ili kukopa na kuwainua kiuchumi.

“Halmashauri yetu imekasimia shilingi milioni 98 kwaajili ya kukopesha vikundi vya wanawake,Viajana na walemavu kutoka mapato ya ndani kama Sera inavyosema na kuwa fedha hizo zinatolewa bila riba na ni kwa mwaka mmoja marejesho ili wengine wakakope”alisema Mgeta.

Mgeta aliongeza kuwa changamoto wanayokuimbana nayo ni vijana waliowengi kutopenda kufanyakazi na kama  wanafanya kazi hawapendi kuungana kama kikubdi na kama wanaungana wanabagua kazi za kufanya.

Mgeta alitumia nafasi hiyo kuwataka wale wote bwanaokuja kukopa wajifunze na tabia ya kurejesha ili wengine nao wakakope na kuwa fedha hizo nizatolewa kwa mzunguko lengo ni kuwainua wananchi kiuchumi.

 Nye mwenyekiti wa CCM Wilaya Rorya,Charles Ochere alipongeza halmashauri ya Rorya kwa kuitikia wito wa Rais awamu ya Tano,John Pombe Magufuli kujali makundi haya kwa kuwakopesha fedha ya makusanyo ya ndani ili kujikwamua kiuchumi.

Ochere aliongeza kuwa hapo nyuma walikuwa na ugomvi na halmashauri kwa sababu ya kushindwa kuwatekelezea wananchi mahitaji yao na kuwa chanzo kikuu kilikuwa hicho cha kushindwa kuwakjopesha wakina mama,Vijana na walemavu.

Naye mwenyekiti wa UVCCM Wilaya Rorya Daud Mwita aliwataka vijana kuchangamkia frusa kama hizo pindi zinazojitokeza kwasababu zinakuja mara chache na watakao kuwa wa kwanza ndio watakaofanikiwa.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.