Header Ads

Vyeti vya kuzaliwa sasa kutolewa kwa Mtendaji Kata


Mkurugenzi  wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma Godwin Kunambi amesema Halmashauri hiyo itahakikisha watoto wote wenye umri chini ya miaka mitano wanasajiliwa kwa ajili ya kupatiwa vyeti vya kuzaliwa bure kutokana na umuhimu wa nyaraka hiyo ambayo kuanzia tarehe 15 Machi, 2019 itaanza kutolewa katika Ofisi zote za Kata 41 za Jiji hilo na katika baadhi ya vituo vya kutolea huduma za Afya.

Akizungumza na wataalam hao katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Umonga, Kunambi aliwataka wawajibike kikamilifu katika kufanikisha huduma hiyo kwa Wananchi ili kila mtoto mwenye haki ya kupata cheti hicho katika Jiji la Dodoma apatiwe.

Kwa upande wake Mratibu wa zoezi hilo katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma Aneth Mwambya alisema mafunzo hayo ni siku tatu na kuanzia Machi 11, 2019 na kwamba  kuanzia Machi 15, 2019 zoezi la usajili wa watoto na utoaji wa vyeti vya kuzaliwa  litaanza katika ngazi ya Kata.
“Tunatoa wito kwa kila mzazi mwenye mtoto mwenye umri wa chini ya miaka mitano wafike katika Ofisi za Kata na katika baadhi ya vituo vya kutolewa huduma za Afya zinazotoa huduma ya mama na mtoto ili wasajiliwe kwa ajili ya kupatiwa vyeti hivi vya kuzaliwa” alisema mratibu huyo.

Alisema zoezi hilo litaanza kwa kampeni ya siku 12 kuanzia Machi 15, 2019, na baada ya muda huo huduma hiyo itaendelea kutolewa kama kawaida, na kwamba kila mzazi atatakiwa kuwasilisha nyaraka za awali zikiwemo Tangazo la kuzaliwa kwa mtoto au kadi ya kliniki kabla ya mtoto husika kusajiliwa na kupatiwa cheti.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.