Header Ads

Waalgeria wanamtaka Rais Bouteflika ajiuzulu


Maelfu ya waandamanaji wamekusanyika katika mji mkuu wa Algeriakudai kumtaka kujiuzulu mara moja kwa rais wa nchi hiyo Abdelaziz Bouteflika licha ya kutangaza kuwa hana nia ya kugombea tena kiti hicho kwa muhula mwingine. Jumatatu ,aliahirisha uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika tarehe 18 Aprili.

Waandamanaji hata hivyo wanamshutumu rais huyo mwenye umri wa miaka 82 kwa kurefusha zaidi muhula wake kinyume cha sheria.

Wanafunzi wamekuwa wakiongoza maandamano makubwa dhidi ya Bouteflika ambayo yameingia siku ya tano sasa.

Rais huyo ambaye ni mgonjwa huonekana kwa nadra sana hadharani na hajawahi kuhutubia umma tangu alipopata kiharusi mwaka2013.

Alirejea nchini mwaka mapema wiki hii baada ya kulazwa katika hospitali nchini Uswiss.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.