Header Ads

Wangabo atahadharisha vitendo cya kuchelewesha kusikiliza mashauri


RUKWA:Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ametahadharisha vitendo vya kuchelewesha kusikiliza  mashauri mbalimbali katika baraza la ardhi na nyumba la Wilaya ya sumbawanga hali inayowapelekea wananchi kuhisi kuhusisha ucheleweshaji huo na vitendo vya rushwa na hivyo kuwataka kushikamana na kutafakari kauli mbiu ya wiki ya sheria yam waka huu iliyowataka kutoa haki kwa wakati kwa kushirikiana na wadau.
Amesema kuwa pamoja na mkoa kuwa na baraza moja la wilaya kati ya wilaya zake tatu na hivyo kupelekea kuelemewa na mashauri yanayotoka katika wilaya nyingine za mkoa hiyo isiwe sababu ya wajumbe wa baraza hilo kuchelewesha mashauri jambo ambalo limekuwa likilalamikiwa na wananchi kwa muda mrefu.
Ameyasema hayo katika hafla fupi ya kumuapisha mjumbe wa baraza la ardhi na nyumba la wilaya ya Sumbawanga Bi. Leticia Sami, ambapo kwa sasa Mkoa wa rukwa una baraza moja tu la ardhi na nyumba ambalo linapatikana katika wilya ya Sumbawanga.

Kwa upande wake mwenyekiti wa baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ya Sumbawanga Bi. Frida Hamis Chinuku amesema kuwa mchakato wa kumpata mjumbe huo unaanzia kwa majina kupendekezwa na Mkuu wa Mkoa na kisha majina hayo kupelekwa kwa Waziri mwenye dhamana ambapo humteua mjumbe na hatimae mjumbe huyo kuapishwa.  

Kiapo hicho kinatokana na maelekezo ya Kanuni za mwaka 2003 za Sheria ya namnba 2 ya utatuzi wa migogoro ya ardhi ya mwaka 2002.


Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.