Header Ads

Watu 126 wapoteza maisha kusini mwa Afrika

Mvua kali zilizoambatana na kimbunga zilizojiri nchini  Afrika kusini, Msumbiji na Malawi zimesababisha watu 126 kupoteza maisha.

Mvua hizo kali zilizoambatana na kimbunga zimeathiri zaidi ya watu 800 na kusababisha zaidi ya watu laki moja kuyahama makazi yao.

Kimbunga hicho pia kimeharibu miundombinu kwa kiasi kikubwa na hasa mfumo wa umeme.

Mashirika mengi ya misaada ya kimataifa yameanza kutoa misaada kwa waathirika, huku kazi za uokoaji na utafutaji pia zikiendelea.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.