Header Ads

Wavuvi waaswa kufungua akaunti maalumu ya wavuvi ili kuondokana na changamoto hiiDar es salaam:Kutopatikana kwa mikopo ya kutosha na yenye masharti nafuu kwa wavuvi  imetajwa kama changamoto ya sekta hiyo kutokufikia malengo ambapo wavuvi wameaswa kujitokeza na  kufungua akanti maalum ya wavuvi ili kuweza kutatua changomoto hiyo.

Hayo yamesemwa na Banki ya Posta TPB ambayo imepanga kushiriki katika kukuza uchumi wa nchi kupitia sekta ya uvuvi kwa kuwapa hamasa wananchi wanaojishughulisha na sekta hiyo.Kufuatia kuwepo kwa changamoto hiyo banki yaTPB nchini leo imezindua akanti kwa ajili ya wavuvi yenye lengo la kutambua mchango wa sekta hiyo katika kukuza uchumi wa nchi na kuwapa hamasa zaidi wananchi wanaojishughulisha na uvuvi  katika  kujiwekea akiba pia kutumia huduma za kibenki ili kurahisisha shughuli zao za kila siku.

Akizungumza kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa akaunti hiyo, mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya benki ya TPB Dkt. Edmund Mndolwa amesema katika mazungumzo ya awali kati ya TPB na chama cha wavuvi  benki hiyo iliathimia kuwapatia wavuvi elimu ya fedha, uwekaji wa akiba na kuwapatia mikopo midogo midogo kwa ajili ya kununua vifaa vya uvuvi kama vile injini za maboti.


Naye mwenyekiti wa chama cha wavuvi bw. Alphonce Mkama amesema akaunti hiyo maalum itawawezesha wavuvi kujiwekea akiba na pia kuwawekea mazingira maalum ya kuwawezesha kuendeleza shughuli zao.Inakadiriwa kuwa Tanzania ina wavuvi zaidi ya milioni nne (4), na kati ya hao ni wavuvi 56,000 ndio wanachama waliojiunga na vyama vya wavuvi, hivyo ushirikiano huo utafungua njia kwa wavuvi ambao si wanachama kujiunga kwenye vyama vilivyopo maeneo yao ili waweze kufikiwa kirahisi na huduma za kibenki.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.