Header Ads

Waziri jafo atoa maagizo haya kwa mtendaji mkuu wa wakala wa mabasi yaendayo haraka
DAR ES SALAAM: Waziri wa nchi  ,Ofisi ya raisi Tamisemi Suleiman Jafo amemuagiza Mtendaji mkuu wa wakala wa mabasi yaendayo   haraka Mhandisi Leonard Lwakatare  kuhamishia Mabasi kumi  yanayobeba abiria kutoka mbezi kwenda kimara  katika barabara ya mwendo kasi inayoanzia kimara hadi kivukoni na Gerezani 


Akizungumza  na  Wandishi  wa Habari Mara baada ya kufanya ziara fupi katika eneo la kivukoni  katika mradi huo jijini Dar es Salaam  Waziri   Jafo amesema kutoka na adha iliyojitokeza hiv karibu iliyotokana na baadhi ya mabasi hayo kuharibika amesema mabasi matano yahamishiwe  kimara kivukoni na mengine Matano yatakuwa ya kimara gerezani. 

Aidha Jafo amemtaka Lwakatale kuhakikisha kuwa UDART ambaye ndiyo kampuni yenye dhamana ya kusafirisha abiria kuhakikisha  inafanya matengenezo ya mara kwa mara ya mabasi yake ili kuondoa usumbufu unaojitokeza wa kupungua kwa mabasi na kunakosababisha  mabasi mengi kuwa mabovu.

Katika hatua nyingine Waziri Jafo ameiagiza Dart kuwasiliana na Sumatra ili mabasi ya kawaida yaongezwe katika eneo la kimara mpka mbezi ili kutatua adha ya usafiri katika eneo hilo mara baada ya mabasi hayo kumi kupungua .


Wananchi wameahidiwa kujulishwa mambo yote muhimu yanashughulikiwa kwa lengo la kuwawezesha wananchi kushiriki vema katika kujenga uchumi kupitia huduma bora ya usafiri itakayoboreshwa

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.