Header Ads

WFP waungana na TRC kusafirisha chakula nje ya nchi


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Issack Kamwele amesema hawezi kuwa tayari kuona baadhi ya masuala yanashindwa kufanikiwa katika taasisi zilizo chini ya wizara yake kwa kisingizio cha kubanwa na sheria.


Alisema hayo wakati wa hafla yaa kutiliana saini mkaataba wa kutengenezaa mabehewa 40 kati ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) kwenye karakana ya treni jijini Dar es Salaam.


Mhandisi Kamwele alisema, uwiano wa mizigo inayosafirishwaa hailingani na uwezo wa maamlaaka ya bandari na TRC kutokana na uwekezaji mkubwa uliowekwa na Serikali ya Awamu ya Tano na fursa ya kupakana na nchi zisizo na baahari.

"TRA (Mamlaka ya Mapato Tanzania), TPA (Mamlaka ya Bandari Tanzania) na TRC zinakwamisha uwezo wa bandari yetu kupakua naa kupakia mizigo. Tutafanya hiki kwa pamoja maaana nimebaini tatizo kubwa lipo TRA,” alisema Mhandisi Kamwele na kuongezaa:

"Nimeshamwandikia baruaa Waziri wa Fedha na Mipango tukutane kwa ajili ya maazungumzo, maana sheria za fedha zipo lakini kama zinatukwamisha tuzifanyie marekebisho. Kwa mfano Uganda inazalisha tani laki 7.5 kwa mwaka lakini uwezo wa bandari yetu hadi sasa ni tani laki tatu kwa mwaka, tunakwama wapi. Tutataajana naani anakwamisha kupaata hii mizigo.”

Aidha, katika hafla hiyo TRC na WFP walikubaliana kusafirisha mizigo yaa chakula kutoka shirika hilo la kimataifa linalosambaza chakulaa ndani na nje ya nchi.

Ambapo katika kuimarisha uhussaano wao WFP wameamua kutoaa kiasi cha Dola za Kimarekani 600,000 sawa na Sh Bilioni 1.1 kwa ajili ya kukarabati mabehewa 40 ya shirika hilo.

“Napenda kutumia furssa hii kuwashukuru WFP kwa msaada huu ambao utaenda kukuza uwezo wa shirika la reli katika kuhudumia mizigo hususan unaopita bandari ya Dar es Salaam kwenda mikoa mingine na nchi jirani kama Uganda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Zambia, Rwanda na Burundi. Tunashukuru WFP kwa kuungaa mkono juhudi za serikali iliyojielekeza kuleta mageuzi ya kiuchumi chini kwa kukuza biashara na kujenga uchumi wa viwanda,” alisema Mhandisi Kamwele.

Katika kuimarisha shirika hilo, hivi karibuni Rais Dk. John Magufuli alitoaa kiasi cha Bil 4 kwa ajili ya ukarabati wa maabehewa ya mizigo, ambapo lengo ni kukarabati mabehewa 200 hadi kufikia sasa TRC wameshakarabati mabehewa 40.

Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa alisema kwa kiasi kikubwa mabadiliko yametokea ndani ya shirika hilo tangu kuingia madarakani Rais Magufuli, ambaye aliapa kuinua uchumi wa watanzania kupitia viwanda na miundombinu imara.

"Miaka 15 iliyopita TRC ilikuwa na uwezo wa kusafirisha hadi tani milioni 1.4 kwa mwaka, lakini katikati tulipata misukosuko tukapoteza uwezo wetu. Tulipolibinafsisha tulizifunga njia nyingi katika reli ya kati na ya Tazara.

"Tunafanya ukarabati mkubwa katika reli ya kati, tunakarabati kilomita 970. Tayari kipande cha Tanga hadi Mombo kimeshakamilika viwanda vya saruji vimeanza kusafirisha mizigo yao kwa njia ya reli,” alisema Kadogosa.

Alibainisha, uhusiano wao na WFP unafikia mwaka mmoja sasa na kwa kuwa hilo ni shirika la kimataifa kuna uwezekano mkubwa wakapata wateja wengi zaidi kwa kuwa vigezo wanavyotumia kutaka kusafirisha mizigo hadi vimekubaliwa maana yake TRC wanaweza kufanya kazi na shirika lolote duniani.

“Mkakati huu wa kukarabati mabehewa una lengo la kukarabati mabehewa zaidi ya 500, kwa sasa tunaanza na haya 200 kwa fedha iliyotolewa na Rais Magufuli. Tunafanya kazi usiku na mchana ili tumalize mapema, mpango huu utasaidia kutoa ajira za moja kwa moja 30 na za muda mfupi 32,” alisema Kadogosa.

Kwa upande wake Meneja Mkazi wa WFP, Michael Dunford alisema walianza kutoa kazi za muda mfupi ili kuangalia uwezo wa TRC lakini ndani ya kipindi kifupi wamevutiwa na uwezo wao na ndiyo maana wameamua kufanya nao makubaliano.

Ushirikiano huu utakuwa na tija kwa wakulima na wafanyakazi wa kubeba na kupakua mizigo kuanzia bandarini hadi kwenye maeneo ya reli, kwa kuwa WFP wamepanga kuwa watanunuaa chakula kutoka Tanzania ambayo ni faida kwa wakulima na watasafirisha kwa kutumia miundombinu ya reli na wakifika maeneo ya maziwa makuu watavusha kwa kutumia Ziwa Victoria kwenda nchi jirani.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.