Header Ads

Askari jeshi la zima moto afukuzwa kazi kwa kuhusika na vitendo vya rushwaDODOMA:Jeshi la zimamoto na ukoaji limemfukuza kazi askari mwenye namba US/ZM 2946 FC Joseph Chale kutokana na kuhusika katika vitendo vya rushwa na unyanyasaji kwa wachimbaji wadogo wa madini wilaya ya Chunya mkoani Songwe.

Hatua hizo zinachukuliwa dhidi ya maafisa na askari waliohusika katika vitendo vya rushwa na unyanyasaji kwa wachimbaji wadogo wa madini huko Chunya mkoani Mbeya  mwishoni mwa mwezi Machi ,2019.
  
Kamishina wa operesheni jeshi la zimamoto na ukoaji Billy Mwakatage juzi  jijini hapa amewaambia waandishi wa habari kuwa wapo maafisa na askari wengine ambao bado shauri lao liko kwenye mahakama za kijeshi kwa utaratibu  na kanuni za jeshi la zimamoto na ukoaji.


Hata hivyo jeshi la zimamoto na ukoaji linatoa wito kwa wananchi kutoa taarifa kwa makamanda wa zimamoto na ukoaji wa mikoa pindi wanapokutana na vitendo vyovyote wanavyovitilia shaka hususani kwenye shughuli za ukaguzi wa kinga na tahadhari dhidi ya moto unaofanywa na maafisa na askari  wa jeshi letu.

Mwisho. 

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.