Header Ads

Diwani kata ya Bahi ampongeza Rais Mafufuli kwa hili
Na   Jackline Victor Kuwanda 
DODOMA: Diwani wa kata ya Bahi  Bwana  Augustino  Ndonu amesema kuwa kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt John Pombe Magufuli ya kuwa na elimu Bure imekuwa na msaada mkubwa katika kata yake kwani mwitiko wa wazazi katika kuwapeleka watoto shule umekuwa mkubwa .

Ndonu ameyasema hayo wakati akizungumza na kituo hiki ambapo amesema kuwa, serikali ya awamu ya tano imeweza kuondoa wananchi katika vikwazo mbalimbali  hasa kwa upande wa michango.


Aidha, ameongeza kuwa wakati anaingia kwenye uongozi,   alikuta kuna changamoto ya upatikanaji wa maji , hivyo ameishukuru serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt John Pombe magufuli kwa kumpatia fedha kwaajili ya kutatua changamoto hiyo.


Mbali na hilo amesema kuwa serikali ya awamu ya tano haitaki mtu anaye tembea polepole, bali inamuhitaji mtu anaye fanya kazi , kwani mh Rais anahitaji mtu anaye chapa kazi na ambaye anakubali kuongea na watu wa chini.


Hatahivyo, Bwana Ndomu amebainisha changamto ambayo inaikabili kata hiyo ikiwemo changamoto ya miundombinu ya umwagiliaji kwani daraja lililoko pale limekuwa likisababisha matatizo kwa wananchi.Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.