Header Ads

Faida zitokanazo na kusamehe

Msamaha ni kuondoa uchungu wote ulioulimbikiza ndani ya moyo wako kwa hiari yako mwenyewe. Wakati mwingine kubeba uchungu ndani ya nafsi yako unakufanya ushindwe mpaka kufanya vitu vya maendeleo.

Au kwa maneno mengine tunaweza kusema neon msamaha ni kitendo cha kurudisha uhusiano wa awali uliovunjika, na kuanza mahusiano mapaya pasiana na kinyongo chochote kile.  Kusamehe ni kumfutia mtu makosa yake aliyokutenda bure kabisa.

Hizi ndizo ni faida za kusamehe:-

Tunasamehe kwasababu kusamehe ni tabia ya Mungu. Tunapaswa kusameheana kwani muasisi wa msamaha ni Mungu mwenyewe, na kama Mungu angehesabu maovu yetu nani angesimama? Hayo ni maneno kutoka katika vitabu vya Mungu, hivyo kila wakati tunapaswa kuelewa na kutambua na kuelewa nguvu iliyopo katika msamaha ili mioyo yote iweze kuwa salama.


Tunasamehe ili tuweze kusamehewa. Unapaswa kusamehe kwa faida yako mwenyewe siyo kwa faida ya mkosaji. Mwachie Mungu apambane na watesi wako wala usilipe kisasi.

Unasamehe ili uwe na amani. Unaposamehe unakuwa unapata amani ya moyo. Mtu ambaye anavumilia uchungu ulioumbika ndani ya moyo na hataki kuachilia fundo hilo lazima litamtesa na atakosa amani ya moyo. Atahangaika na huku uchungu ulioumbika ndani ya moyo ukiendelea kumtafuta.

Unasamehe ili uwe na furaha. Kwa kweli ukiangalia watu wanaokataa kusameheana huwa hawana furaha kabisa katika mioyo yao. Kama unaishi katika mahusiano yoyote na mara nyingi huwa watu si wakamilifu basi msamaha ndiyo kiunganishi chenu ambao utarudisha uhusiano uliopotea

Tunasamhe ili tuwe na afya njema
Uponyaji wa kweli unaanzia moyoni. Kama mtu anasamehe kutoka moyoni basi huo ni msamaha wa kweli na ni msamaha unaoongozwa na  “huruma ya Mungu ndani yake” Watu hawataki kusamehe ndio maana wengine afya zao ni dhaifu. Uchungu ulioumbika ndani ya moyo unaendelaa kuwatafuna.

Mwisho unatakiwa kukumbuka, usizeeke kabla ya wakati kwa ajili ya kutosamehe watu wengine

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.