Header Ads

Hawawezi kuzungumzia maendeleo, watakuwa wanajitia Kisu cha tumbo - Makamu wa Rais


Makamu wa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu amesema kuwa alisikia dondoo za Magazeti mtu akihoji ulinzi wa Rais baada ya kutafakari kazi kubwa anayofanya.

Samia amesema kuwa hii inaonyesha jamaa zao wameishiwa (pasipo kuwataja ) huku akisema kuwa hawawezi kuzungumzia maendeleo kwasababu watakuwa wanajitia kisu cha tumbo kwasasa wanajiweka katika kuhoji vitu ambavyo havihitaji kuhojiwa.

Makamu wa Rais ameyasema hayo leo, wakati wa hafla ya uzinduzi wa mji wa Serikali uliopo Ihumwe mkoani Dodoma.

Samia amesema kuwa “Nilisikiliza dondoo za magazeti na kusikia mtu anahoji kuhusu ulinzi wa rais, nikajiuliza anahoji ulinzi ili iweje kwa nini asitumie muda huo kuhoji maendeleo yanayoendelea.”

“Hii inaashiria kwamba jamaa zetu wameishiwa, wamefilisika na mawazo na nini wazungumze ndani ya nchi yetu, kwa sababu hawawezi kuzungumzia maendeleo haya watakuwa wanajitia kisu cha tumbo kwa hiyo sasa wanajiweka katika kuhoji vitu ambavyo havihitaji kuhojiwa, ila Watanzania tuko na wewe.”

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.