Header Ads

Hii ndio sababu inayo sababisha watu wengi kushindwa kufanya biashara

Watu wengi sana wanafikiria kuingia kwenye biashara, lakini ni wachache sana ambao wanafanikisha malengo yao ya kuingia kwenye biashara. Wengine huendelea kufikiria kwamba iko siku mambo yatakwenda vizuri na hatimaye wataingia kwenye biashara.

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao umekuwa ukisema utaingia kwenye biashara miaka nenda miaka rudi unatakiwa kuelewa kwamba kuna baadhi ya vitu vinavyokuzuia wewe kuingia kwenye biashara. Na bila ya kutatua vitu hivi kwanza utajikuta siku zinakwenda na biashara huanzi.

Watu wengi husingizia vitu viwili vikubwa ambavyo vinawazuia kuingia kwneye biashara;

Kitu cha kwanza ni mtaji.
Kila mtu atakuambia napenda sana kuingia kwenye biashara lakini mtaji sina. Mwaka wa kwanza mtaji huna, mwaka wa pili mtaji huna, inaendelea hivyo mpaka miaka mitano au kumi unaimba wimbo mmoja mtaji sina? Unafikiri ni kweli?

Kitu cha pili ni wazo bora la biashara.
Hapa napo watu wengi husema wanakwama, hawajui ni biashara gani wafanye ambayo itawalipa na kuwaletea mafanikio. Habari njema ni kwamba mawazo ya biashara yapo kila sehemu na yapo mengi sana. Na habari njema zaidi kwako ni kwamba tumeandika kitabu PATA WAZO LA BIASHARA, kukipata bonyeza hayo maandishi.

Kama kikwazo cha wewe kuingia kwenye biashara sio mtaji ambao umekuwa unapigia kelele kila siku na wala sio wazo bora maana yapo kila mahali, ni nini sasa? Ni kitu gani hiko kimekuwa kinakuzuia wewe kuingia kwenye biashara na kuweza kutimiza ndoto zako?

Jibu linakuja kwenye kitu kimoja tu,Haupo tayari kuanza na kidogo.
Kila unapopanga kuingia kwenye biashara unafikiria mtaji wa mamilioni, unafikiria wazo ambalo litatengeneza biashara ambayo itakuwa kubwa sana na itawafikia wengi. Vizuri sana kwa kuwa na mawazo haya makubwa. Lakini je unawezaje kufikia hayo makubwa kama hutaanza kidogo?

Utawezaje kufika ngazi ya kumi kama hutaanzia kwenye ngazi ya kwanza? Mtoto atazaliwaje akiwa anatembea, anaongea na anajua kila kitu? Mwanafunzi ataanzaje shule siku ya kwanza na hapo hapo apewe mtihani na kufaulu?

Unaona hata asili yenyewe inakwenda kinyume na mawazo yetu ya kuanzia juu. Kila kitu kwenye maisha kinaanzia chini. Mti mkubwa kama mbuyu ulianza na mbegu, na kuna wakati ulikuwa kama mchicha.

Ni vizuri sana kuwa na mawazo makubwa kwa biashara yako, ila hakikisha una sehemu ya kuanzia kidogo. Anza kidogo sana kwa uwezo ambao upo ndani yako. Mwanzoni mwa biashara utahitaji kuweka juhudi za ziada, kujibana na kuwa na maisha ya tofauti.

Hata kama biashara unayotaka kufanya bado huwezi kupata mtaji wa kuanzia chini, angalia biashara nyingine unayoweza kuanzia chini na kisha ukatengeneza mtaji wa kuingia kwenye biashara unayotaka.

Usipoteze muda wako mzuri kwa kufikiri kwamba biashara ni lazima ianze ikiwa kubwa ndio uonekane unafanya biashara. Anzia chini kabisa na hapa utajifunza mambo mengi sana kuhusu biashara yako. Na kama utakuwa makini utakua vizuri na biashara yako na hatimaye utafikia malengo yako ya kuwa na biashara kubwa.

Anzia chini, weka juhudi, jifunze na endelea kukua. Hii ndio njia itakayokufikisha kwenye malengo yako makubwa ya kibiashara.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.