Header Ads

Huu ndio mpango wa serikali kwa vijanaNa Jackline Victor Kuwanda 
DODOMA:Naibu Waziri wa Vijana ,Kazi na Ajira , kupitia ofisi ya waziri Mkuu  ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Antony Peter mavunde amesema kuwa kupitia ofisi  hiyo imekuwa ikisimamia sera ya vijana na  moja kati ya sera kubwa ni kuwawezesha vijana .

Mavunde ameyasema hayo wilayani chamwino mkoani Dodoma mbele ya wajumbe wa kamati ya katiba na sheria waliofika wilayani  humo ili kujifunza namna ya uuandaaji ,utunzaji na undelezaji wa vitalu nyumba (GREEN HOUSE).

Aidha, Mavunde ameongeza kuwa serikali ina mpango wa kuhakikisha kuwa katika mwaka huu wa fedha inawapatia mafunzo vijana 18,800 nchini, kupitia  mafunzo ya uandaaji  wa kitalu nyumba pamoja na shamba Darasa  ili kuwajengea uwezo  vijana wa vijana kujiajiri  na kuajirika kupitia mafunzo hayo.


Mbali na hilo Mavunde amesema kuwa hivi sasa vijana tayari wamepata mafunzo  na wanauwezo wa kutengeneza vitalu nyumba na kampuni imeanza kuwatumia vijana hao  nje ya mpaka wa mkoa wa Dodoma .


Mh Najma  Giga ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba na Sheria  ambapo amewapongeza vijana  kwa kujikita katika kilimo na kuwaomba vijana hao  waendelee kuwahamasisha vijana wengine wa tanzania ili kazi hiyo iweze kuleta tija.


Chipegwa Albert John pamoja na Ezekiel Festo Masima ni miongoni mwa vijana walio waliopata mafunzo hayo na ni miongoni mwa vijana waliopata nafasi ya kutembelea Halmshauri zote za Mkoa kwenda kueneza ujuzi ili waliopata ili wenzao nao waweze kupata ujuzi huo na wakatoa pongezi kwa Serikali ya Awamu ya tano kwa kuwawezesha vijana.Wakati huo huo wajumbe wa kamati ya katiba na sheria walitembelea chuo cha Mtakatifu Don Bosco kilichopo Jijini Hapa, ambapo waliweza kujionea kwa namna ambavyo wanafunzi wa chuo hicho wameweza kunufaika na baadhi ya miradi   ambayo serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania inaendeesha hapa nchini  ambayo ni  programu ya ukuzaji ujuzi inayosimamiwa chini ya ofisi ya waziri mkuu kwa ajili ya kuwaweza vijana.


Akisoma Risala mbele ya kamati hiyo Mkuu wa chuo cha Don Bosco  Padri Boniface Nchami amesema kuwa lengo la chuo hicho ni kuwasaidia vijana wote wenye malengo ya kuweza kunyanyua ujuzi wao na kuendelea na ujuzi wao ili waweze kujipatia ajira au kujiajiri.Mh mavunde amesema kwasababu wanaenda katika uchumi wa viwanda waliona ni vyema wakaandaa nguvu kazi ambayo itasaidia kupata ujuzi ambao utawapa sifa ya kuweza kujiajiri na kujirika.Kwa upande wake Naibu waziri wa ofisi ya waziri mkuu anayeshughulikia walemavu stella ikupa amesema kuwa serikali ambayo inaoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli pamoja na changamoto ya ajira kwa vijana lakini serikali ilivyo sikivu imeendelea kuhakikisha kuwa kundi la vijana wa kitanzania linaondolewa katika changamoto ya ukosefu wa ajira.Najma giga amesema hilo ni jambo la faraja kubwa kwa wazazi pamoja taifa kwani mbali na changamoto ya ajira lakini serikali pamoja na vyuo hivyo binafsi wimeweza kujitahidi  kupunguza changamoto hiyo.


Nao wanafunzi wa chuo hicho wameishukuru serikali kwa kuwasaidia vijana kwani progarmu hiyo waliyo ipata imeweza kuwasaidia katika maisha yao.


Hatahivyo, Nia ya serikali ni kuona kuwa vijana wengi wanapata uwezo wa kuweza kujiajiri katika sekta mbalimbali kuaminika na makampuni mbalimbali kufanya kazi kwa juhudi na maarifa na hivyo kuwa chachu ya maendeleo kwa jamii na serikali kwa ujumla.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.