Header Ads

ICC yatishia kuwawajibisha viongozi wa mapigano Libya


Mwendeshamashtaka mkuu wa ICC ametishia kuzidisha uchunguzi kwa Viongozi wa pande zinazohasimiana Libya, baada ya taarifa kuwa idadi ya waliokufa imepindukia 140, na wengine 18,000 wameyakimbia makaazi yao.

Takwimu hizo za hasara iliyosababishwa na uhasama mpya uliozuka nchini Libya zimetolewa na msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric, akinukuu ripoti ya shirika la kimataifa la kuwashughulikia wahamiaji, IOM.

Ripoti hiyo inasema raia 13 ni miongoni mwa watu 146 waliokwishauawa katika mapigano hayo yaliyoanza Aprili tano, lakini Dujarric ameeleza bayana kuwa idadi hiyo ni ya wale tu ambao vifo vyao vimethibitishwa, ikimaanisha kuwa yawezekana idadi ya wahanga wa vita hivyo ni kubwa zaidi.

Msemaji huyo wa Umoja wa Mataifa amesema wahamiaji wasiopungua 3000 wamenaswa katika vituo walimozuiliwa, ambavyo vipo karibu na uwanja wa mapambano, ametoa rai kwa pande zinazohusika kujizuia.

Tunazitolea mwito pande zote zinazohusika kusitisha uhasama, ili angalau tuweze kuwafikishia msaada wa kibinadamu watu wanaouhitaji mjini Tripoli. Tunapata taabu kubwa kuwafikia watu, kwa sababu magali ya kubeba wagonjwa na ya wafanyakazi wa afya yameshambuliwa, na hilo halikubaliki. Tunataka pande zote kurudi katika kutafuta suluhisho la kisiasa.'' Amesema Dujarric.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.