Header Ads

Ikupa-serikali inaendelea na jitihada zake za kuhamasisha wadau mbalimbali kuandaa na kutekeleza programu za kukuza ajira nchini


DODOMA:SERIKALI imesema sekta binafsi nchini imechangia kuziba pengo la ajira kwa kuzalisha ajira 137,054 sawa na asilimia 28, huku sekta ya umma ikiongoza kwa ajira 345,547 sawa na asilimia 72.
Kiwango cha juu cha uzalishaji wa ajira katika sekta ya umma kinatokana na utekelezwaji wa miradi ya maendeleo.
Taarifa ya Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi na Wenye Ulemavu,  Stella Ikupa, imeeleza kuwa serikali inaendelea  na jitihada zake za kuhamasisha wadau mbalimbali kuandaa na kutekeleza programu za kukuza ajira nchini.
Naibu Waziri huyo alikuwa akizungumza na watu wenye ulemavu na wadau mabalimbali wakati wa tamasha la uimbaji lililoandaliwa na Tanzania Music Foundation linalofanya kampeni ya kupinga unyanyasaji na vitendo vya ukatili kwa watu wenye ulemavu.
Kwa mujibu wa Ikupa, sekta hizo zilichangia kupunguza pengo hilo la ajira katika mwaka wa fedha 2017/2018.
Alisema kutokana na jitihada hizo za serikali kwa watu wenye ulemavu wameweza kupatiwa ajira na wengine kuwezeshwa kwenye ujasiliamali na hivi sasa na kufanikiwa kujitegemea kama ilivyo kwa wengine wasiokuwa na ulemavu.
Aidha alisema kuwa kwa kuhakikisha watu wenye ulemavu wanaondokana na baadhi ya changamoto walizokuwanazo,serikali pia haitawaacha nyuma kimaendeleo bali itaendela kuwawezesha kuishi maisha ya kujitegemea kwa kuwa tayari imeshatunga sheria ya fedha ya mwaka 2018.
Alisema kuwa sheria hiyo ikiwa ni ya kuzitaka halmashauri zote nchini kutenga asilimia mbili ya fedha za mapato ya ndani kwa ajili ya kuwawezesha watu wenye ulemavu katika shughuli za kiuchumi ambapo mikopo hiyo utolewe bila riba yoyote.
“Hapa ninatoa wito kwa wezangu watu wenye ulemavu kote nchini kuchangamikia fursa hiyo iliyotolewa na serikali kupitia halmashauri zake,ninaowaomba muunde vikundi vya ujasiliamali ili mnufaike na fedha hizo zilizotengwa”alisema.
Naibu waziri huyo hata hivyo alisema kuwa ni ukweli usiopingika kupitia matamasha mablimbali ya uimbaji yamekuwa yakiisaidia serikali katika uelimishaji kwa jamii juu ya kupinga vitendo vya unyanyasaji na ukatili wanaofanyiwa watu wenye ulemavu.
“Ni ukweli hapa nikiri kuwa bado elimu kwa jamii inahitajika kwa kupitia njia mbalimbali,kutokana na changamoto nyingi kama vile zinazowanyima haki za kimsingi ikiwemo elimu,ajira pamoja na huduma za marekebisho kwenye muindombinu mbalimbali ya majengi ambayo siyo rafiki kwa watu wenye ulemavu”alisema.
Naye kwa upande wake Rais wa Tanzania Music Foundation Dk Donald Kisanga,akisoma risala kwa Naibu waziri huyo,ameiomba serikali kuhakikisha inatoa ajira kwa watu wenye ulemavu kwa wale wenye sifa ya elimu na ujuzi ili kuwapunguzi makali ya changamoto walizokuwanazo.
Alisema kuwa pamoja na serikali kuhamasisha taasisi,mashirika na watu mbalimbali,katika upande wa sekta ya ajira kwa watu wenye ulemavu bado ni changamoto hivyo imewafanya kuendela  kutangatanga mitaani na vyeti vyao.
Mbali na hilo Rais hiyo pia ameiomba serikali kuwachukulia hatua kali kwa wazazi wanaoendelea kuwaficha  na kuwafungia watoto wenye ulemavu ndani na kuwanyanyapaa kwa kuwanyima haki zao za msingi ikiwemo elimu,afya,chakula na mavazi.
Kisanya akisoma risala hiyo kwa Naibu waziri huyo kwenye tamasha hilo,aidha ameiomba serikali kuhakikisha mauaji ya albino yanakomeshwa,ikiwa na pamoja kuwachukulia hatua kwa wale wanaochafua mazingira kwa kuwa kunahatarisha maisha kiafya ya watu wenye ulemavu hasa kwa wale wanaotambaa.
MWISHO.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.