Header Ads

Italia kusaidiana na Tanzania kuboresha huduma za utengamao kwa watoto


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Italia nchini Tanzania Bw. Roberto Mengoni katika ofisi za Wizara zilizopo Jijini Dodoma.

Katika maongezi hayo Balozi huyo amesema Serikali ya Italia itasaidiana na Serikali ya Tanzania katika kuboresha huduma za utengamao kwa watoto kwa kuhakikisha kila kituo cha afya kinakua na jengo maalum litakalotumika katika kuboresha afya za watoto hao wenye matatizo ya akili.

Kwa upande wake Waziri Ummy amesema Serikali imeshaanza kujenga majengo hayo na kuhakikisha kila kituo cha Afya kinakua na chumba kwa ajili ya Utengamao.

Sambamba na hayo, Waziri Ummy amesema Serikali itahakikisha inaajiri watumishi watakaokua na uzoefu wa kazi hiyo ili kuweza kuleta ahueni kwa wazazi na walezi wenye watoto wenye matatizo ya akili.

Katika kuhakikisha hilo linafanyika, Waziri Ummy amemuagiza kamishna wa Ustawi wa Jamii Bw. Naftal Ng'ondi kuwasiliana na wataalam wa michoro wa wizara ili waweze kuchora michoro ya majengo yatakayotumika kama vyumba vya utengamao katika ngazi zote za utoaji wa huduma za afya nchini.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.