Header Ads

Jabiri Bakari azishauri Taasisi za umma kuendelea kutumia vizuri TEHAMADODOMA: WAKALA ya Serikali Mtandao Umetengeneza mfumo shirikishi wa kusimamia shughuli za rasilimali za Taasisi(ERMS) utakaoboresha mazingira ya utendaji kazi ndani ya taasisi.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dodoma mtendaji mkuu wa wakala huo JABIRI BAKARI amesema mfumo huo unaunganisha shughuli mbalimbali za taasisi kuwa katika mfumo mmoja unaowezesha usimamizi,ufuatiliaji,ukaguzi na tathimini ya utekelezaji wa shughuli zote za taasisi kwa ufanisi.
Amesema mfumo huo wa ERMS una moduli kumi na nane zinazounganisha shughuli mbalimbali za utendaji kazi zinazotegemeana na kuwezesha kubadilisha taarifa miongoni mwa idara au vitengo na kusimamia rasilimali kama vile watu,vitendea kazi na fedha.
Amezishauri taasisi za umma kuendelea kutumia vizuri TEHAMA katika kuboresha utendaji kazi serikalini na utoaji wa huduma za umma kwa kuzingatia mingozo na viwango vya serikali mtandao vinavyopatikana katika tovuti ya wakala huo.
Mbali na mfumo huo wakala pia ulishatengeneza mifumo mbalimbali ikiwemo mfumo wa Malipo ya Serikali Kielektroniki(GePG)kwa kushirikiana na wizara ya Fedha na Mipango ambao ndio wasimamizi wakuu wa mfumo huo .
    

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.