Header Ads

Jumuiya za Maji zaagizwa kuongeza mtandao wa Maji


Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam amewaagiza Jumuiya za watumia maji Kuwaunganishia maji wananchi kwa Mkopo na walipe ndani ya miezi sita hadi mwaka.

Ametoa maagizo hayo leo wakati wa ziara ya kutembelea miradi ya pembezoni inayohudumia wananchi ambao hawapo kwenye mtandao wa DAWASA.

Akizungumza baada ya kutembelea miradi ya jumuiya za watumia majii  na namna wanavyotoa huduma ya maji kwa wananchi Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema kuwa, angependa kuona wananchi wengi wanahudumiwa na jumuiya hizo hiyo amewaagiza waendelee na mchakato wa kuwaunganishia maji kwa njia ya mkopo wa miezi sita hadi mwaka mmoja.

Luhemeja amesema, mbali na kuwaunganishia maji wananchi kwa mkopo pia wapunguze bei ya maji na kufikia bei elekezi 1663 kwa Ujazo wa Lita 1000 ili kuwa na uwiano sawa wa bei za maji kwa wateja wote.

 “Kwa sasa hivi huduma za Jumuiya ya watumia maji zote zitakuwa chini ya DAWASA, kwahiyo tunawataka bei za maji ziweze kupungua tunafahamu kuna changamoto zinawakabili ila tutakaa chini kati ya idara inayosimamia miradi yenu na jumuiya ili kuweza kuweka kila kitu sawa wananchi wapate maji kwa bei elekezi,”amesema Luhemeja.

Amesema kwa sasa wanaendelea kuvipitia visima vyote vilivyopo kwenye jumuiya za watumia maji ambazo vilijengwa na Dawasa, serikali, wadau wa maendeleo mbalimbali na jamii yenyewe na kukagua ubora wa maji ikiwemo na kujenga Water Treatment Plant kwa ajili ya kuweka maji dawa.

 Luhemeja ameeleza kuwa, wateja wote waliounganishwa kwenye miradi hiyo jamii wataingizwa kwenye mfumo wa malipo wa Kieletroniki na watalipia kupitia mitandao ya simu ili kuboresha mapato ya kila mwezi.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.