Header Ads

Kauli ya Kamanda Muroto 'Watapigwa na watachakaa' yatua bungeni


Mbunge wa Viti Maalumu Chadema, Devotha Minja katika swali la nyongeza amehoji juu ya Makamanda wa Polisi wanaotumia lugha za vitisho kwa wananchi kama ile iliyotolewa jana na Kamanda Muroto ya 'Watapigwa watachakaa'.

Mbunge huyo ameihoji serikali kuwa kazi ya msingi ya Jeshi la Polisi kwa wananchi wanaolipa kodi ni kuchakazwa.

”Si wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya tu ambao hawafanyi vizuri wapo pia ma RPC ambao hawafanyi vizuri, mwenyekiti RPC anapotangaza kwamba wananchi wakiandamana atawapiga hadi wachakazwe, hivi kazi ya msingi ya Jeshi la Polisi kwa wananchi wanaolipa kodi ili walipwe mishahara kazi ya msingi ni kuchakaza wananachi,” amehoji Devotha leo Bungeni jijini Dodoma.

Akijibu swali hilo Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo "Nadhani kitu kikubwa kama Taifa ni kuweka ushirikiano katika kila eneno nadhani vyombo vingine vinaongozwa kwa mujibu wa sheria kanuni na taratibu katika suala zima la Mambo ya Ndani na sitaki kuingilia. Wananchi wote tutafuata utaratibu wa utii wa sharia na taratibu bila shuruti, ili kuepuka migongano inayoonekana sio ya lazima."

Kauli hiyo imekuja baada ya jana, Kamanda wa Polisi Dodoma, Gilles Muroto ambaye alitoa tahadhari kwa wananchi ambao leo April 9, 2019 walipanga kufanya maandamano ya amani kupinga azimio la bunge kuhusu kufanya kazi na CAG kupigwa na kuchakazwa wakifanya hivyo.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.