Header Ads

Kocha wa Simba SC alia na Ratiba ya Ligi KuuKocha wa Simba SC, Patrick Aussems ameonesha kilio chake dhidi ya ratiba ya michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) kutokana na kuwa na viporo vya michezo mingi vilivyokutokana na ushiriki wa timu yake kwenye michuano Klabu Bingwa Afrika.

Patrick amefafanua kuwa wanatakiwa kucheza michezo 8 ndani ya siku 19 huku michezo hiyo ikiwa katika mikoa tofauti hivyo watatakiwa kusafiri kwa umbali mrefu, huku hofu yake akiionesha kwanye afya za wachezaji.

‘Tumerudi kwenye TPL..michezo 8 ndani ya siku 19, Safari na usafari havijajumuishwa( Tanga, Bukoba, Mwanza, Musoma, Morogoro, Mbeya) ratiba sio ya uhalisia! Vipi kuhusu afya za wachezaji?’’ amehoji kocha huyo kupitia mtandao wa Twitter

Leo Simba SC itakuwa mgeni wa Coastal Union kwenye Uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga kwenye mcheo wa Ligi Kuu. Hadi sasa timu hiyo ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi ikitanguliwa na Yanga SC na Azam FC.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.