Header Ads

Kufa au kupona Serengeti Boys leo dhidi ya Uganda


Timu ya taifa ya Tanzania kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 Serengeti Boys leo inatuma karata yake ya pili na muhimu ya mchezo wa kuwania taji la mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri wa miaka 17 sambamba na kukata tiketi ya kucheza Kombe la dunia kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 nchini Brazil.

Serengeti Boys itakipiga na Uganda katika mchezo wake wa pili wakiwa na majeraha wote ya kupoteza michezo yao ya kwanza Kundi A, timu itakayopoteza hapo itaaga rasmi mashindano hayo na kusubiri mchezo wa kukamilisha ratiba tu ya michuano hiyo.

“Nimepata muda wa kukaa na vijana kwa maana ya kuongea lakini kufanyika mazoezi kidogo japokuwa hauwezi ukafanya mazoezi ya nguvu, kwa vyovyote vile tutataka kucheza na wachezaji bora tuliokuwa nao ambao pia tunaamini kuwa wanaweza wakafanya vizuri zaidi kama ambavyo wengine wanafanya ili kupata matokeo” alisema kocha wa Serengeti Boys Oscar Mirambo mbele ya waandishi wa habari.

Mara ya kwanza na mwisho kwa Tanzania kushiriki michuano hii ilikuwa 2017 nchini Gabon na iliaga mashindano haya kwa kupoteza kwa goi 1-0 dhidi ya Niger ambao walifuzu kucheza nusu fainali na fainali za Kombe la Dunia, hivyo kama Tanzania itashinda itarejesha matumaini ya kukata tiketi hiyo na kama itashindwa.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.