Header Ads

Kutolewa kwa Juventus UEFA kwatibua rekodi ya Cristiano Ronaldo


Kwa mara ya kwanza Cristiano Ronaldo anaikosa Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya tangu mwaka 2010.

Hii inamaanisha kuwa baada ya miaka 9 hatutomuona  Ronaldo katika UEFA Champions hatua ya nusu fainali baada ya hapo jana timu yake ya Juventus kutupwa nje ya michuano hiyo na Ajax hatua ya robo fainali.

Kwa miaka 9 mfululizo Ronaldo akiwa na Madrid alifanikiwa hatua ya fainali mara 4 na kuishia nusu fainali mara 5.

Kwa upande mwingine baada ya kufunga goli moja usikuwa jana, Cristiano Ronaldo sasa ametimiza magoli 126 katika Champions League. magoli 65 kati ya hayo amefunga katika hatua za mtoano, hiyo ni idadi kubwa kuliko mchezaji yeyote.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.