Header Ads

LHRC wasaini makubaliano na Ubalozi wa Norwey nchini


Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimesaini mkataba wa makubaliano na Ubalozi wa
Norwey nchini ili kusaidia katika kuendeleza shughuli za kupigania haki za binadamu ikiwemo haki
ya uhuru wa kujieleza.

Mkurugenzi wa LHRC, Anna Henga amesema lengo lao kubwa ni kutetea haki za binadamu na wanapenda sana kutetea utawala wa kisheria nchini Tanzania.
Kwa upande wake Balozi wa Norway nchini, Eizabeth Jacobsen amesema wamesaini makubaliano na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu ili wandeleze kutoa elimu na uelewa wa masuala ya haki za binadamu kwa wananchi kwani siyo kila mtu anaelewa maana ya haki za binadamu.

"Uhuru wa kujieleza uko mashakani sehemu nyingi ulimwenguni, ni jukumu letu sote kuhakikisha tunapigania haki ya uhuru wa kujieleza ili haki zingine za binadamu zisiendelee kuminywa," amesema Balozi huyo.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.