Header Ads

LHRC yaiomba serikali na watanzania kuendelea kusimamia haki za binadamu


DAR ES SALAAM: Kituo cha Sheria na Haki za binadamu (LHRC kimeiomba Serikali pamoja na watanzania kwa ujumla kuendelea kusimamia haki za binadamu na kuunga mkono juhudi za utetezi wa haki hizo kwa lengo la kujenga jamii yenye haki na usawa.

Rai hiyo imetolewa   jana Jijin Dar es salaam na Mkurugenzi wa kituo hicho Anna Henga wakati wakisaini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano na Serikali ya Norway kupitia ubalozi wa Norway hapa nchini.

Anna amesema ni jukumu la kila mmoja kuhahakikisha anafuata na kulinda sheria za haki za binadamu ili kujenga nchi yenye nguvu, umoja na ushirikiano katika safari ya kuelekea uchumi wa kati hususani watu wenye ulemavu, watoto na wanawake ambao wamekuwa ni wahanga wakubwa kunyimwa haki zao.


Aidha amesema lengo kuu la kituo cha Sheria na Haki za binadamu ni kuifikia jamii yenye Haki na Usawa katika kufikia lengo hilo, wameandaa na kutekeleza malengo mkakati kuwezesha kuratibu kazi za utetezi wa haki za binadamu.


Pia amesema wanamshukuru balozi wa Norway nchini Elisabeth Jacobsen kwa kufadhili mpango mkakati wao kwani makubaliano hayo yatawajengea nguvu katika utetezi wa haki hasa kwa kuzingatia kwamba changamoto ya ukiukwaji wa haki za binadamu imeendelea kuwepo nchini.Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.