Header Ads

Lipumba awataka wakina mama,vijana wa chama chake kujiandaa kwa uchaguzi mkuu
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF, Prof. Ibrahim Haruna Lipumba amewataka wakina mama na vijana wa chama hicho visiwani Zanzibar kujiandaa na uchaguzi Mkuu ifikapo mwaka 2020.

Hayo aliyasema jana wakati akizungumza na viongozi wa ngazi wa matawi, majimbo, wilaya na Taifa wa chama hicho katika ukumbi wa Judo ndani ya uwanja wa Amani Mjini Magharib Unguja.

Prof.  Lipumba alisema wakina mama na vijana wa chama hicho ndio wenye jukumu kubwa la kuimarisha uhai wa chama visiwani humu na kwamba kwa wakati huu ndio ni muda wa kujiandaa na uchaguzi mkuu ifikapo mwaka 2020.

"Wakina mama na vijana nyinyi ndo wenye chama mnatakiwa kukijenga kwa kuimarisha umoja kati yenu kwa ajili ya uchaguzi mkuu ifikapo mwaka 2020, lengo letu ni kuingia katika serikali ya Zanzibar kupitia Umoja wa kitaifa,"alisema Mwenyekiti huyo.

Mbali na hilo, Mwenyekiti huyo alisema kuwa viongozi wahahakikishe kuwa ifikapo mwaka 2020 Chama cha CUF hivyo kinapaswa kuiongoza Serikali kwa kuzingatia sera yake ya haki sawa kwa wote.

Mwenyekiti huyo aliwataka Viongozi na wanachama kuacha majungu na maneno yasiyo na msingi na kwamba wajikite katika kukijenga chama kwa kueneza sera na falsafa ya haki sawa kwa wote ili  kuwavutia wale waliotoka ndani ya chama kurudi na kuimarisha Chama hicho.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.