Header Ads

Maafisa ugani 100 wapatiwa elimu mkoani njombeMaafisa ugani 100 mkoani Njombe wamepata elimu ya upimaji wa udongo kwa lengo la kufahamu aina za udongo katika maeneo yao ili kuweza kumsaidia mkulima katika matumizi bora ya mbolea.

Afisa Ugani wa Kampuni ya OCP inayofanya kazi ya  Upimaji wa udongo pamoja na Uuzaji wa Mbolea Joshua Ivan Joel akizungumza na Muungwana blog mara baada ya kutolewa mafunzo hayo  katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Njombe amesema  Wakulima wengi wamekuwa wakifanya kilimo cha Mazoea bila kupima Udongo na baadaye hujikuta wanaingia katika hasara kubwa kwa kuwekeza gharama kubwa katika kilimo huku mavuno yake yakishindwa  kuakisi gharama za uzalishaji.

“nisahihi kufanya vipimo vya udongo ili kuweza kumsaidia mkulima atumie mbolea gani na kwa kiwango gani kutokana na mazingira husika na ukiangalia ardhi ya Njombe ina upungufu wa virutubisho tofauti tofauti kutokana na maeneo mbali mbali ndio maana tumeanzisha upimaji wa udongo unatofautiana kwa acidic,alkalinity na virutubisho vingine ndio maana tunatoa elimu hii ili tuanze zoezi la upimaji udongo”alisema Joshua joel

Naye afisa kilimo  kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Njombe Stela Julius Kutona anasema kupitia zoezi hilo wanatarajia wakulima kwenda kulima kibiashara zaidi.

“kama mkoa tunatarajia kupitia hili zoezi wakulima wetu wataenda kulima kibiashara zaidi tofauti na awali ambapo walikuwa wakilima kilimo cha mazoea bila kujua udongo wake unahitaji mbolea gani wala kiasi gani matokeo yake wanapata mavuno madogo na kupata pesa ya kujikimu pekee”alisema afisa kilimo

Baadhi ya Maafisa Ugani  walioshiriki Mafunzo hayo wamekiri kuwa wakulima wengi wamekuwa wakilima kilimo cha mazoea huku wakisema kuwa Elimu ya kilimo bora bado inahitajika kwa wakulima huku wakishukuru zoezi la upimaji ardhi litakalofanyika mkoani Njombe kwa kuwa itawasaidia wakulima kujua namna ya kutumia mbolea katika maeneo yao.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.