Header Ads

Maelfu waandamana Australia dhidi ya sera ya wahamiaji ya nchi hiyo


Maelfu ya watu wamekusanyika katika miji mbalimbali ya Australia katika maandamano nchini kote dhidi ya sera kali ya serikali kuhusu wakimbizi pamoja na huduma isiyoridhisha wanayopewa waomba hifadhi nchini humo.

Maandamano hayo yaliandaliwa na Jumuiya ya Waislam ya Canberra, yanapinga uwepo wa vituo vilivyopo nje ya Australia vya kuhifadhi wahamiaji katika visiwa vya Nauru na Manus ambapo mamia ya wakimbizi wanaotaka kuingia nchini humo wamekuwa wakipelekwa huko tokea mwaka 2013.

Diana Abdel Rahman, Rais wa shirika lisilo la kiserikali la Australian Muslim Voice amesema huduma wanayopata wakimbizi katika kambi hizo ni mbaya kuliko wanayopewa wanyama.

 Maafisa wa serikali wamesema kwa sasa kuna takribani wakimbizi na waomba hifadhi 915 katika visiwa vya Nauru na Manus.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.