Header Ads

MAGUFULI ATENGUA NA KUSAMEHE NJOMBENJOMBE: Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.John pombe Magufuli amemtengua na baadaye kumsamehe mkuu wa polisi wilaya ya Njombe kutokana na mauaji ya watoto yaliyotokea miezi miwili iliyopita mkoani Njombe na kusababisha doa kubwa Nchini na nje ya Tanzania.

Rais Magufuli ametoa uamuzi huo mkoani Njombe wakati akizungumza na wananchi mkoani humo katika uwanja wa sabasaba mjini Njombe.

Aidha Rais Magufuli amesema kuwa endapo yatatokea mauaji hayo kwa mara nyingine mkuu wa mkoa pamoja na viongozi wengine watawajibishwa.

Hata hivyo Rais Magufuli aliomba mchungaji yeyote kuongoza Toba kwa mkutano huo huku naye akishiriki toba na kuamua kumsamehe OCD huyo.

Awali mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka  aliomba radhi kwa niaba ya wananchi huku akimueleza Rais wale wote waliohusika na mauaji ya watoto wamekwishafikishwa mahakamani

Katika hatua nyingine Magufuli amemkabidhi mkuu wa mkoa wa Njombe rambi rambi kiasi cha shilingi milioni 5 kwa ajili ya familia zilizokumbwa na matatizo hayo.

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.