Header Ads

Makonda atimiza ahadi yake kwa wajane

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda leo ametimiza ahadi yake aliyoitoa juzi ya kuwapatia wajane kiasi cha Shillingi milioni 10 za kusaidia kutatua changamoto za kiofisi zilizokuwa zikiwanyima usingizi wajane ikiwemo ya malimbikizo ya madeni ya kodi kwenye nyumba wanayoitumia kama ofisi.Itakumbukwa juzi wakati wa kongamano la wajane RC Makonda alitoa ahadi ya kuwapatia milioni 10 na kuwatafutia eneo la kujenga jengo la ofisi za makao makuu ya chama cha wajane Tanzania na tayari eneo limepatikana tayari kwa ujenzi.

Mapema Leo Afisa elimu wa Mkoa wa Dar es salaam, Hamis Lissu amewakabidhi Milioni 10 kwa niaba ya RC Makonda ambae yupo katika majukumu mengine ya Kitaifa.

Kwa upande wao wajane wamemshukuru RC Makonda kwa kuwasaidia kutatua changamoto mbalimbali zilizokuwa zikiwakabili na wanaamini kupitia uongozi thabiti wa RC Makonda ujenzi wa jengo la makao makuu ya chama hicho utakamilika kwa uharaka. 

Get it on Google Play

No comments:

Powered by Blogger.